Ndugu zangu,
Kuna mengi yametokea katika siku za karibuni. Ni mengi yenye kuhitaji tafsiri. Nitaanza na hili lililomkumba David Kafulila ambalo kimsingi ni mgogoro unaoendelea ndani ya NCCR- Mageuzi.
Katika dunia ya magari ya kizamani usiombe unase kwenye gea ya reverse. Kutoka kwake ni shughuli pevu. NCCR – Mageuzi imenasa kwenye gea ya reverse. Ni gea ya kurudia nyuma.
Ishara zilishaonekana. Kilichotokea ndicho kilichokuwa kinasubiriwa. Kilichotokea ndani ya NCCR- Mageuzi si kwamba chama kimemfukuza mwanachama, bali, kundi moja ndani ya chama limefanikiwa kumfukuza mwanachama mwenzao.
Tumemwona Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Sam Ruhuza akitamka kwenye TBC1, kuwa NCCR- Mageuzi inaona uchungu sana kumpoteza Kafulila. Kwamba NCCR- Mageuzi wanawatunza wabunge wao kama mboni ya jicho. Naam, katika siasa, alichofanya Sam Ruhuza ni kutoa machozi ya mamba.
Na tukaambiwa haraka, kuwa NCCR- Mageuzi sasa imeomba kwenda Ikulu kukutana na JK kuhusiana na Katiba. Tafsiri; Kafulila ndiye aliyekuwa akipanga magogo kwenye njia ya kwenda kwa JK, pale Ikulu ya Magogoni .
Tulidhani , baada ya purukushani ile ya mpaka mwanachama tena mbunge mwandamizi katika chama kunyang’anywa kadi, NCCR- Mageuzi wangeianza safari ya kwenda kwa wanachama na wapenzi wao. Kufanya mikutano ya ndani na nje kuwaeleza kilichotokea na kujibu maswali n a hoja za wanachama na wapenzi wa chama hicho.
Ndugu zangu,
Kinachotokea ndani ya NCCR- Mageuzi ni mgogoro wa ndani ya chama. Inahusu kuwania mamlaka ya uongozi wa chama na inaweza kuunganishwa, kwa mbali, na mbio za urais wa 2015. Hilo la mwisho linahitaji uchambuzi wake.
Na kinachotokea NCCR- Mageuzi ni pigo na huzuni kwa tunaopenda uwepo wa siasa za upinzani wa vyama vingi hapa nchini. Hofu yangu siku zote ni pale itakapotokea, CCM ikaondoka madarakani na kuiacha Chadema ikishika hatamu za dola huku tukiwa na CCM dhaifu kama chama cha upinzani na vyama vingine aina ya NCCR- Mageuzi na CUF vilivyojifia kwa kujitundika vyenyewe vitanzi vya ’ CCM B na CCM C’. Kuna ishara zinazonyesha hatari ya kufika huko.
Kwa hapa tulipo, NCCR- Mageuzi inahitajika kama chama kamili na kinachoaminika cha upinzani. Tulipo sasa kila mbunge wa upinzani na hususan kila sauti ya mbunge wa upinzani yenye kujenga ni muhimu sana katika bunge ambalo walio wengi ni Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi. David Kafulila alikuwa ni mmoja wa watu hao.
Sam Ruhuza wa NCCR- Mageuzi anajua, kuwa katika siasa tunaamini kila kitu kinawezekana. Hivyo basi, kama hakukufanyika jitihada zozote za kumbakisha ndani ya chama David Kafulila, mwanasiasa huwezi kusimama na kusema unaona uchungu kumpoteza mbunge wenu.
Na hapa tunajifunza, kuwa wakati umefika wa kuangalia upya taratibu za kuwapata na kuwavua ubunge wabunge wetu. Umefika wakati tuweke katika Katiba yetu mpya. Kuwa mbunge aliyechaguliwa na wananchi , hata kama atafukuzwa uanachama wa chama chake, bado atabaki kuwa ’ Mbunge Pori’ mpaka uchaguzi utakaofuata. Kwamba hatutakuwa na uchaguzi mdogo.
Kinahitajika nini kwa sasa NCCR- Mageuzi?
Usuluhishi, usuluhishi, usuluhishi. Ni usuluhishi utakaopelekea Kafulila kumaliza muda wake wa Ubunge. Na Msajili wa Vyama John Tendwa hawezi tu kusimama pembeni na kuongea na media kwamba kufukazana kwenye vyama ni ufisadi. Ndio, Tendwa hawezi kuingilia mambo ya ndani ya NCCR-Mageuzi, lakini, kama mlezi wa vyama vya siasa, Tendwa anaweza kushiriki kazi ya usuluhishi. Pamoja na mgogoro uliopo kati ya David na James ifike mahali wawili hao wasaidiwe kutanguliza hekima. Kwamba wawili hao , James Mbatia na David Kafulila, waishi kwa kuikubali hali hadi 2015. Maana, baada ya hapo, kama hawatapata muafaka wa kwao wenyewe na wa kirafiki, basi, mmoja wao lazima atoke zizini.
Na kikubwa, NCCR- Mageuzi watangulize maslahi ya taifa. Wakae sasa kama chama. Watambue kuwa chama kina mgogoro mkubwa. Kama Tendwa atashindwa kuwasaidia, waombe mtu au watu wenye hekima waende wakafanye kazi ya usuluhishi. Ndio, David na James wanahitaji kusuluhishwa. Maana, kikubwa hapa ni kuwafikiria pia wananchi wa Kigoma Kusini wenye kuhitaji uwakilishi wa mbunge wao waliomchagua.
Nape Nnauye Naye?
Alianza vema kuzichanga karata za kisiasa kwa kinachotokea NCCR- Mageuzi. Gazeti Tanzania Daima linamnukuu Nape akisema kuwa; ” Sipendi tabia ya kuwafukuza wanasiasa wanaohoji mambo na hasa wakiwa vijana. ” Hapo Nape alicheza haswa karata za siasa huku akiligeukia kundi kubwa la vijana waliokipa mgongo chama chake.
Lakini, kama ilivyo mgema ukimsifia sana. Nape anamalizia vibaya kuchanga karata zake za siasa kwa kusema; ” Nakishukuru Chama cha NCCR- Mageuzi kwa kuturudishia jimbo letu, nina uhakika wa jimbo hilo kurudi CCM”.- (Nape Nnauye, Tanzania Daima, Desemba 20, 2011.)
Ni kauli hiyo ya Nape inayokinzana na kauli yake ya ; ” Nchi kwanza, Chama Baadae”. Nape angepaswa kufahamu, kuwa kwa NCCR- Mageuzi kumfukuza Kafulila kwa sasa ni suala lisilo na maslahi kwa nchi. Angesubiri sana kuzungumzia chama chake kitakavyonufaika na jambo hilo.
Ni tafsiri yangu tu.

No comments:
Post a Comment