|
Euzebia Nickolas |
Euzebia Nickolas huyu ni mwanafunzi wa chuo CBE Dododma akiwa katika pozi la uzuni ni baada ya kutolewa katika chumba cha mtihani kwa kile kilichosemekana kutoonekana kwa jina lake katika orodha ya wanaotakiwa kufanya mtihani. Akieleza MIWANI BLOG kuwa yeye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili na anashangazwa na tukio hilo kwani tayari ameshakwisha fanya mitihani iliyopita na mbona jina lake lilikuwepo. Hali hii imewashangaza baadhi wa wanafunzi wa chuoni hapo na ndipo kila mmoja akiongea na MIWANI BLOG kwa nyakati tofauti walieleza mapungufu makubwa yaliyopo katika chuo chao hali ambayo inawafanya kuwa na migomo ya mara kwa mara hali mabayo ilishatishia kusimamishwa kwa baadhi ya wanafunzi chuoni hapo na hatimaye viongozi wa juu wa serikali kuingilia suhala hilo. MIWANI BLOG ilitafuta njia ya kuonana na mkuu wa chuo lakini palikuwa patupu kwani Msaidizi wa chuo aliliambia Mtandao wa MIWAN BLOG kuwa Mkuu wa chuo hayupo na yeye hana mamlaka wa kulizungumzia hilo ndipo mwanahabari wetu alipo mtwangwa swali msaidizi huyo kwa kumuuliza Je? pakitokeaa jambo lolote ambalo litakuwa limesababisha na kuzuuliwa kwa mwanafunzi huyu kutofanya mtihani hutalizungumzia mpaka mkuu awepo. Na katika hali ya ukali tena kwa kutupa mgongo alijibu kwa kusema " Nimeshasema kuwa mimi sio msemajo mkuu subiriri mpaka atakapo rudu mkuu kwani mlivyokuja mlinifata mimi au mlikuja kumfata mkuu wa chuo" katika hali ya mshangao na kutopata jibu la kueleweka tukirudi mtamboni na maoni ya wanachuo bila ya kupata jubu lolote kuhusu suhala zima la kukosekana kwa jina la msichana huyo na baada ya muda uongozi ulimruhusu kufanya mtihani huku wakilishughulikia suala hilo, Hapo palokuwa na utata juu ya suala la kufanya mtihani na na kushughulikiwa kwa tatizo hilo hii ni maoja ya matatizo yanayoteakea katika baadhi ya Taasisi za elimu ya juu chini kwetu na huku wanafunzi wakiiomba sereikali kutoa kauli ya ukali kukemea tatizo hiloambaloo huwa linajitokeza mara kwa mara na kuwataka chuo kuweka kumbukumbu zao kwa uhakika zaidi ipasavyo na sio kubuni tu. Hadi tukindoka katika eneo la tukio hali ilikuwa sallama na hakuna vurugu zozote zilizotokea. Habari na Mwanahabari MIWANI BLOG - DODOMA
No comments:
Post a Comment