Thursday, 15 December 2011

Bern Ruta 
Bern Ruta
Tanzania yenye wanyama wengi na hifadhi kubwa.Hiki nacho kilikuwa kama ni kivutio kimojawapo kisichojieleza maana hata Watanzaia wengi walikuwa hawajawai kujiuliza lakini ilitokea kwa rafiki wa kigeni baada ya kutembelea jengo linaloitambulisha Tanzania nchini India na kumkuta Twiga mweupe , mnyama ambaye ni moja kati ya wanyama wanaoitambulisha nchi yetu, kama ilivyozoeleka kuwa mnyama huyo ana rangi ya nyano na mabaka meusi lakini yeye alikwishakuwa mweupe hili lilikuwa ni sehemu ya kufanya wengi kujiuliza kama sio kutaka kuja kumuona moja kwa moja kwa macho yao, lakini walipokuwa kituliza wenyeji wao ni jinsi gani na ni katika mbuga gani kila mmoja alikutwa na kigugumizi hali amboya ilimpelekea mmoja wa wadau wa kubwa wa fani aya Uchoraji na ni mwanamuziki kujitwisha ndoo ya rangi na kumwagia twiga huyo. fatilia michoro ifuatayo

Bern Ruta
Huyu ndiye BERN RUTA, kijana anyeishi New Delhi akiwa katika pozi tofauti kuhakikisha anaifuta taswira isiyo ya kweli katika nchi yake akiwa amevaa flana ya nchi yake ili mradi tu kuonyesha uzalendo na upendo ndani ya moyo wake juu ya nchi yake. Itakuwa si vibaya kwa kumpongeza kwa jukumu zito alilolichukua siku chache kabla ya sherehe za Uhuru, MIWANI BLOG nayo inapenda kukuzawadia tuzo kwa kukupa hongera Mr Bern na MUNGU akuzidishie nguvu za kuipenda Nchi yako pamoja na kuilinda afya yako ili uweze kufikia malengi .

Wasanii wa fani hii wanajua ni jinsi gani ilivyokuwa ngumu na kwa maelezo mafupi na mahojiano ya muda mchacha baina ya Mr Bern na MIWANI BLOG alitupa machache . ilichukua muda wa siku tatu kuweza kumpaka rangi huku akishirikiana na Mchoraji mwenzake Emmanueli.wakiwa katika jukumu hilo zito kila mmoja kwa njakati tofauti alionyesaha jitihada zake ili kuweza kumaliza kwa wakati shughuli nzima ukiachilia mbali majukumu mengine waliyokuwa nayo.


Bern Ruta
Emmanueli

  1. Picha kushoto ni Emmanueli    akiendelea na uchoraji huku akijaribu kutafakari jambo hii ni sehemu ya mawazo tu yanayowatokea wachoraji wakiwa katika kazi zao

Huu ni sehemu ya pozu za uchoraji kwa hali ya utulivu kabisa bila ya kutingisika Camera yetu ilimuekea Emmanueli akiwa katika jukumu hilo zito kwa upande aliofikia. Nasi twesa HONGERA KAKA 




 Picha kulia na kushoto ni Mr Bern akimmalizia twiga aliyekuwa mweupe na sasa kurudia katika hali yake halisi.
Swali linakuja ikiwa kama kawaida ya wachoraji kuweka saini katika michoro yao je? Tanzania haitakuwa na Twiga aliyewekwa saini kama vile tulivyokuwa na Twiga mweupe. Mpaka MIWANI BLOG tunarudi mtamboni hutapata jibu kutokana na simu za wachoraji hao kuwa hazipatikani kwa muda. Ila ikiwa kama kawaida ya MIWANI BLOG kuwa ni miwani kwa jamii tutalifatilia na kuwaletea majibu.

No comments:

Post a Comment