Sunday, 15 January 2012

Hoyce Temu alamba nondoozz


hoyce temu alamba nondoozz!



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe akimtunukia Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa ambaye amewahi kuwa Miss Tanzania 1999 na Mwandishi wa kitabu NAYAKUMBUKA YOTE Hoyce Temu Stashahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Mahusiano ya Kimataifa (Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations) katika Mahafali ya Kumi na Sita ya Chuo cha Diplomasia jijini Dar es Salaam.

Paul Scholes amefunga bao lake la kwanza baada ya 
kurejea tena kuichezea Manchester United ambayo 
imesogea na kuwa na pointi sawa na Manchester City 
baada ya kuilaza Bolton mabao 3-0.

Mkongwe Paul Scholes aifungia Man United bao la kwanza
Mkongwe Paul Scholes aifungia Man United bao
la kwanza
Lakini Scholes, ambaye sasa amefika umri wa miaka 37, alifanikiwa kupachika bao sekunde chache kabla mapumziko baada ya kuunganisha pasi ya pembeni ya Rooney.United ilipoteza nafasi nyingi za kufunga kipindi cha kwanza lakini kazi nzuri aliyoifanya mlinda mlango wa Bolton Adam Bogdan iliisaidia Bolton kuepuka kipigo kikali zaidi. Alifanikiwa kuokoa mkwaju wa penalti uliopigwa na Wayne Rooney katika kipindi cha kwanza.
Bolton ilionekana kuimarika kipindi cha pili na Manchester United walionekana kusinzia kidogo, lakini alikuwa Danny Welbeck aliyeizindua tena Man United kwa kupachika bao la pili kabla ya Michael Carrick kufumua mkwaju wa umbali wa yadi 20 na kuandika bao la tatu.
Matokeo hayo yameonekana kuipa faraja Man United baada ya kupoteza michezo miwili ya Ligi Kuu ya England, pia kuzidi kuipa changamoto mahasimu wao Man City ambao siku ya Jumatatu watasafiri hadi Wigan kuikabili timu hiyo.
Bao pekee alilofunga Frank Lampard mapema katika kipindi cha kwanza, limeiwezesha Chelsea kuipunguzia kasi Sunderland iliyoanza kucharuka baada ya kumpata meneja mpya Martin O'Neill.
Lampard alitumia uamuzi wa haraka kuuwahi mpira na kupachika bao kwa mkwaju wa karibu baada ya fataki aliyoachia Fernando Torres kugonga mwamba na kurejea uwanjani.
Torres, Lampard na Juan Mata wote walikosa nafasi nzuri za kufunga kipindi cha kwanza.
Lakini Sunderland walipata nafasi nyingi kipindi cha kwanza na walikosa nafasi muhimu ya kupachika bao dakika za mwisho ambapo Craig Gardner na Nicklas Bendtner walishindwa kufunga.
Blackburn waliweza kuhimili vishindo licha ya mfungaji wao mashuhuri Yakubu kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika za mwanzo na kutoka eneo la hatari la kushuka daraja kwa mara ya kwanza tangu mwezi wa Septemba kwa ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham.
Mshambuliaji Yakubu alioneshwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya kumfanyia rafu mbaya Danny Murphy.
Lakini wakicheza nyumbani Blacburn walifanikiwa kupata bao la kwanza lililofungwa na Morten Gamst Pedersen kwa mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja kabla ya David Dunn kupachika bao la pili.
Damien Duff aliipatia Fulham bao la kufutia machozi, kabla ya Mauro Formica kuikamilishia kazi Blackburn kwa kuandika bao maridadi la tatu.
Victor Anichebe akiingia mchezaji wa akiba alifanikiwa kuipatia Everton pointi moja baada ya Aston Villa kuonesha kandanda ya ovyo wakicheza uwanja wa nyumbani.
Darren Bent aliipatia Aston Villa bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya Stephen Ireland katika dakika ya 56.
Meneja wa Everton David Moyes aliona hakuna cha kuikomboa timu hiyo bila ya kumuingiza Anichebe ambaye alifanikiwa kuisawazishia Everton baada ya Landon Donovan kumchezesha kwa pasi murua.
Robbie Keane aliingia kipindi cha pili kwa Villa ikiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kwa mkataba wa muda mfupi, lakini hakuweza kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi.
Bao la kichwa la dakika za mwisho lililofungwa na Steve Morison liliisaidia Norwich kushinda kwa kuilaza West Brom mabao 2-1.
Mkwaju wa juu wa Andrew Surman uliiwezesha Norwich kuandika bao la kwanza muda mfupi kabla ya mapumziko wakati West Brom wakionekana kukosa nafasi nyingi za wazi kupachika mabao.
Shane Long alizinduka haraka na kuipatia bao West Brom kwa kwaju wa penalti baada ya Jerome Thomas kuchezewa rafu.
Lakini Morison aliangushia kipigo cha nne mfululizo West Brom kwa kuandika bao la pili.
Liverpool imekosa nafasi ya kuingia katika timu tano bora za juu baada ya kubanwa na Stoke na kuandika sare ya saba kwa michezo iliyocheza uwanja wa nyumbani wa Anfield.
Dirk Kuyt alipoteza nafasi nzuri ya kuipatia bao Liverpool wakati mpira wake wa kichwa ulipotoka nje.
Martin Skrtel alidonyoa mpira wa kichwa dakika za mwisho lakini Liverpool walikuwa wamejipanga zaidi kwa kuachia mikwaju ya mbali ambayo haikuzaa matunda.
Mkwaju alioupiga Matthew Etherington kwa kumlenga mlinda mlango wa Liverpool Jose Reina ulikuwa ni moja ya majaribio machache ambayo Stoke iliyafanya. Hadi mwisho timu hizo hazikufungana.
Tottenham nayo ilikosa nafasi nyeupe ya kufikisha pointi sawa na vinara wa ligi baada ya kubanwa na kutoka sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Wolves.
Steven Fletcher alikuwa wa kwanza kuipatia Wolves bao kwa mkwaju wa karibu baada ya mlinda mlango Brad Friedel kupangua mpira wa kichwa uliopigwa na Roger Johnson.
Luka Modric aliisawazishia Spurs kwa mkwaju wa yadi 20 baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Gareth Bale ambaye alikosa kuuweka mpira wavuni na ukamkuta mfungaji ambaye hakufanya ajizi.
Wolves walijihami vizuri huku mlinda mlango Wayne Hennessey akiokoa michomo ya Aaron Lennon na Jermain Defoe.
Matumaini makubwa ya Tottenham yaliyoanza kuchomoza hivi karibuni ya kushinda ligi baada ya miaka 50 yalivurugika ambapo kama wangeshinda wangekuwa pointi sawa na Manchester zote mbili huko kileleni wakitenganishwa na wingi wa mabao.

Uchina yasema Marekani ni mchokozi


Gazeti la taifa la Uchina limechapisha makala yanayoishutumu Marekani kuwa "mchokozi", katika mvutano unaozidi Mashariki mwa Asia.
Jeshi la Marekani linataka ushirikiano na majirani wa Uchina
Katika taarifa ya ukurasa wa mbele, gazeti la People's Daily, la chama tawala cha Kikoministi cha Uchina, Adimeri Yang Yi anasema ni wazi kuwa mkakati mpya wa ulinzi wa Marekani, unazilenga Uchina na Iran.Makala hayo yanafuatia sera mpya ya ulinzi iliyotangazwa na Marekani, ambayo inasema italenga eneo la Asia.
Adimeri huyo anailaumu Marekani kwa matokeo ya miaka miwili iliyopita, ambayo amesema yanatishia usalama wa Asia.
Hakueleza matokeo yenyewe.
Aliongeza kusema kuwa ni wazi kuona nani ni mchokozi katika usalama wa eneo hilo.
Taarifa hiyo siyo ya serikali, lakini lazima ilipitishwa na serikali kuwekwa ukurasa wa mbele namna hivo.
Sera mpya ya Marekani iliyotangazwa juma hili, inasema mipango ya ulinzi ya Marekani sasa italenga Asia.
Kuna uwezekano wa kushirikiana na Uchina, lakini ilisema haijulikani wazi nini msimamo wa kijeshi wa Uchina.
Kwa hivo Marekani itahakikisha kuwa ina nguvu kuonesha masilahi yake Asia, na itazidisha maingiliano na washirika wake katika eneo hilo.

WATU 50 WAMEFARIKI KATIKA MLIPUKO WA BOMU - IRAQ


Wakuu wa Iraq wanasema mtu aliyejitolea mhanga ameripua bomu na kuuwa watu kama 50, katika shambulio dhidi ya mahujaji wa Kishia katika mji wa Basra, kusini mwa nchi.
Shambulio dhidi ya mahujaji wa Kishia, Iraq
Polisi walieleza kuwa mahujaji hao walikuwa wanaelekea msikiti mkubwa wa Washia nje ya Basra, mwisho wa ile wanayoita Arbain, moja kati ya vipindi vinavyoadhimishwa na Washia.
Inaarifiwa kuwa watu 90 wengine wamejeruhiwa.
Askari wa usalama 7 ni kati ya watu waliokufa.
Shambulio hilo linakuja wakati mvutano wa kisiasa unazidi baina ya Washia, walio wengi Iraq, na Wasunii.
Mwezi uliopita, serikali yenye Washia wengi, ilitoa amri ya kumkamata makamo wa rais aliye wa madhehebu ya Sunni, Tariq al-Hashemi, kwa mashtaka ya ugaidi.

MELI YA ZAMA WATU 40 BADO HAWAJAPATIKANA


Wakuu wa forodha wa Utaliana wanasema watu kama 40 bado wametoweka, baada ya meli ya abiria iliyobeba watu zaidi ya 4000 kwenda mrama katika mwambao wa Utaliana.
Meli ilizama Utaliana
 Msemaji wa walinzi wa pwani alieleza inawezekana kuwa watu wengine bado wako ndani ya meli.Shughuli za uokozi zimeendelea kutwa, huku wazamia mbizi wakipekua upande uliozama wa meli hiyo, Costa Concordia.
Abiria wawili kutoka Ufaransa na baharia mmoja kutoka Peru wanajulikana kuwa wamekufa.
Mkuu wa kampuni inayomiliki meli hiyo, Gianni Onorato, alisema ushahidi wa awali unaonesha kuwa meli iligonga mwamba;
nahodha haraka akafuata utaratibu wa kuwatoa abiria melini.
Lakini operesheni ilizuwilika kwa sababu meli yenyewe haraka ilipindukia ubavuni na kuzusha mtafaruku.
Taarifa za karibuni zinaeleza kuwa ofisi ya mashtaka ilimzuwia nahodha baada ya kumhoji.

MBUNGE REGIA ESTELATUS AFARIKI DUNIA


MBUNGE wa Viti Maalumu kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regia Estelatus  Mtema (32), amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha, kupinduka eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani Pwani jana.

Ajali hiyo ilitokea saa 5:30 asubuhi karibu na Sekondari ya Ruvu, wakati mbunge huyo na watu wengine saba, wakisafiri kwa gari aina ya Toyota Landcruiser wakitoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema mbunge huyo alifariki baada ya gari hilo alilokuwa akiendesha mwenyewe, kuacha njia na kupinduka.

Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya Mtema kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla aliona gari lingine likija kasi mbele yake,  katika kujaribu kulikwepa, ndipo gari hilo lilipinduka.

"Wakati akiwa hajalipita gari hilo aliliona gari lingine likija mbele kwa kasi , katika kulikwepa wasigongane uso kwa uso, alitoa gari lake barabarani na kusababisha kupinduka,’’ alisema Mangu.

Regia Mtema.Picha na Sanjito Msafiri na Maktaba
Alisema watu wengine saba  waliokuwa kwenye gari hilo walijeruhiwa, wawili kati yao  hali zao zilikuwa mbaya,  walipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam kwa matibabu zaidi, huku wengine watano, wakiwahishwa Hospitali Teule ya Tumbi Kibaha.

Aliwataja majeruhi waliolazwa Tumbi kuwa ni Lawrence Mtokambali (58), Benadetha Mtema (50), Peter Madesa (50) na Rogers Abdallah(18).

Chadema yatoa tamko
Chadema kilisema kuwa Mtema alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho na Waziri Kivuli wa Kazi na  alikuwa mchapa kazi hodari katika majukumu mbalimbali yakiwepo ya kijamii na kisiasa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Chadema jana na kusainiwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, John Mnyika ilieleza kuwa viongozi wakuu wa chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Katibu Mkuu, Dk Willibroad Slaa, wajumbe wa Kamati Kuu, Wakurugenzi wa chama hicho makao makuu na wabunge, wameshtushwa na kifo hicho na kuungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Chadema kimesema taarifa zaidi kuhusu taratibu za maziko, itatolewa mara baada ya kukamilisha majadiliano kati familia ya marehemu, chama na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kufuatia kifo hicho, mkutano wa Chadema uliokuwa umepangwa kufanyika jana Mjini Kibaha umehirishwa hadi itakapotangazwa wakati mwingine.

Elimu yake
Mtema alizaliwa Aprili 21, 1980. Alisoma elimu ya msingi kati ya mwaka 1989 na 1995. Alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani, Dar es Salaam mwaka 1996 hadi  1999 na kuhitimu kidato cha nne.
Aliendelea kidato cha tano 2002 na sita kati ya mwaka 2000 na 2002 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Machame, mkoani Kilimanjaro.

Mwaka 2003 hadi 2006 alisoma Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) na kupata Shahada ya Maarifa ya nyumbani na Lishe. Baada ya kuhitimu shahada yake, marehemu Mtema alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na Chadema na kuteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Vijana ya chama hicho.

Baadaye aliteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika Kurugenzi ya Mafunzo ya chama hicho, nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum.

JK amtumia rambirambi Mbowe
Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha mbunge huyo.

Katika salamu hizo, Rais ameelezea kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha mbunge huyo na kueleza kwamba, marehemu Mtema  amepoteza maisha akiwa kijana na kwamba pigo hilo si kwa Chadema pekee bali kwa taifa zima.

“Nimepokea kwa masikitiko na huzuni nyingi habari za kifo cha Mheshimiwa Mtema katika ajali ya gari. Siyo kwamba ajali hii imechukua maisha ya kijana bali imelinyang’anya taifa mbunge hodari, na kwa hakika, kifo chake siyo tu ni pigo kwa chama chako bali ni pigo kwa sote na kwa taifa letu kwa jumla.

"Nakutumia wewe binafsi, chama chako na wanachama wake salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo na msiba huu mkubwa," alisema Rais Kikwete kupitia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu.
Gari la Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Regia Mtema alilopata nalo ajali iliyosababisha kifo chake jana, eneo la Ruvu, mkoani Pwani likiwa limeegeshwa katika Kituo cha Polisi cha Mlandinzi, mkoani humo.
Aliongeza: “Napenda ujue kuwa niko nanyi katika msiba huu. Napenda vilevile uniwasilishie salamu zangu za rambirambi za dhati kabisa kwa wana-familia, ndugu na jamaa wa marehemu Mheshimiwa Mtema.

Taarifa hiyo imemwomba Mbowe kufikisha salamu za Rais Kikwete kwa familia ya mbunge huyo na kuijulisha kuwa amepokea habari hizo kwa huzuni kubwa. "Wajulishe kuwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, awajalie uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu kwa sababu yote ni mapenzi yake.








Wananchi wamlilia


Katika kuonyesha kuguswa na kifo hicho mamia ya watu wanaotumia mtandao wa kijamii maarufu kwa jina la ‘Facebook’  walielezea kusikitishwa na kifo hicho huku wakitoa maoni mbalimbali.

 Miongoni mwa maelezo yao ni juu ya maneno aliyowahi kuyazungumza mbunge huyo kijana, ukiwamo ujumbe alioandika katika mtandao huo akiwataka wananchi wamweleze kero zao ili azifikishe katika mkutano ujao wa Bunge.

Ujumbe huo aliouandika Januari 10 mwaka huu na kuungwa mkono na watu 159 ulisomeka hivi;

“Wapenzi, habari zenu kama una kero yoyote unayoona inafaa ikasemewe bungeni au nje ya Bunge na Wabunge na Viongozi wa Chadema basi tupia hapa kero yako. Angalizo; isiwe kero binafsi..., karibuni sana pamoja tunaweza”.

Mtema anakuwa mbunge wa pili wa chama hicho kufariki dunia kwa ajali ya gari, Julai 27, 2008 Mbunge mwingine wa chama hicho Jimbo la  Tarime, Chacha Wangwe alikufa katika ajali ya gari

eneo la Pandambili mkoani Dodoma.

Taarifa ya Chadema ilieleza kwamba mipango ya mazishi ya marehemu inapangwa  nyumbani kwa baba yake, Tabata Dar es Salaam .

Wednesday, 11 January 2012


MBUNGE  wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na wenzake 10 sasa wameiomba Mahakama Kuu Dar es Salaam iiamuru Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi(CUF) wajieleze ni kwa nini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri ya mahakama hiyo.
Ukiacha wadhamini hao, jana Hamad Rashid  na wenzake, waliomba mahakama iamuru pia wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Seif Sharrif Hamad wajieleze kwanini wasitiwe hatiani kwa kukiuka amri hiyo.

Pia wanaiomba mahakama hiyo ibatilishe uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi la  chama hicho wa kuwavua uanachama hapo Januari 4, 2012, kwa madai kwamba walikiuka katiba ya CUF.

Kabla ya uamuzi huo wa kuwavua uanachama, Januari 3, 2012, Hamad Rashid na wenzake waliwasilisha ombi  Mahakama Kuu Dar es Salaama chini ya hati ya dharura wakiomba mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho uliokuwa ukitarajiwa kufanyika Zanziba, uzuiwe kuwajadili.
Kupitia kwa mawakili wao, kampuni ya uwakili ya GF Law Chambers Advocates  walidai baraza hilo lina nia ya ama kuwasimamisha au kuwavua uanachama na kwamba uamuzi huo ungeathiri haki zao za kikatiba.

Waliendelea kudai kwamba, kuna kesi ya msingi ya madai namba 1 ya mwaka 2012  waliyoifungua mahakamani hapo wakihoji muundo wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho   na uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo.
Tayari Jaji Augustine Shangwa katika uamuzi wake wa Januari 4, 2012, aliamuru CUF kusitisha uamuzi wa ama kuwasimamisa au kuwavua uanachama walalamikaji hao.

Hamad Rashid jana alirejea amri hiyo ya mahakama kuu chini ya Jaji  na kueleza kwamba  CUF waliikaidi na badala yake kuendelea na kutekeleza azma yake ya kuwavua uanachama.


Mbunge wa Wawi kwa tiketi ya CUF, Hamadi Rashid Mohamed (mwenye kaundasuti) na wenzake wakitoka Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, jana, kuwasilisha kiapo cha mahakama kwa kulalamikia viongozi wa Cuf walikataa oda ya mahakama hiyo iliyozuia kufanyika kwa mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi wa chama hicho Januari 4. Kushoto ni Shoka Khamis Juma, mmoja kati ya wanachama wanne wa Cuf walivuliwa uwanachama akiwemo na Hamadi. Picha na Said Powa
 
Katika hati ya kiapo cha Hamad iliyowasilishwa mahakamani hapo, alidai  kwamba baada ya mahakama kutoa uamuzi huo, wakili wake akisaidina na mtumishi wa mahakama aliyemtaja kwa jina la Khatibu, waliwasilisha taarifa ya amri hiyo ya mahakama katika ofisi za chama hicho Buguruni saa 6:20 mchana.

Hata hivyo alidai kuwa Ofisa wa chama hicho aliyejulikana kwa jina la Mikidadi Nyandula alikataa kuipokea.
Alidai kwamba,  baadaye saa 6:50 wakili wake alimtumia uamuzi wa mahakama hiyo kwa njia ya baruapepe na kwamba yeye Hamad Rashid aliiwasilisha nakala ya uamuzi huo wa mahakama kwa Afisa Mkuu wa mlalamikiwa saa 8.15 mchama ili aiwasilishe kwa Katibu Mkuu.

Hamad Rashid alizidi kudai katika hati hiyo kwamba,  baada ya kuwasilisha uamuzi huo alitakiwa kufika mbele ya Baraza Kuu saa 8:25  na kutakiwa kujitetea na kwamba, ombi lake la muda wa kuandaa utetezi lilikataliwa.
Alisema pia  aliwaarifu wajumbe wa baraza hilo kwamba mahakama kuu ilikuwa imetoa uamuzi na amri ya kulizuia kuendelea na azma yake.

“Niliwaonesha wajumbe wa baraza hilo waliokuwepo katika mkutano huo nakala ya uamuzi huo,” alisisitiza Hamad Rashid katika kiapo chake hicho.

Alifafanua kwamba  hata hivyo, baraza hilo lilipuuza amri hiyo ya mahakama na kusisitiza kuwa ni lazima achague ama kujitetea mwenyewe au kutoka nje ya mkutano.

“Niliamua kutoka nje ya mkutano ili nisihusike katika kuidharau mahakama,”alifafanua Hamad  Rashid.
Aliendelea kudai kwamba walalamikaji wengine nao waliitwa mbele ya baraza hilo na kila mmoja aliliambia baraza hilo kuwa hawezi kuendelea kwa kuwa kuna amri ya mahakama, ambayo inazuia kuendele na mkutano huo.

“Hivyo, kila mlalamikaji aliwaonesha wajumbe wa baraza hilo nakala ya uamuzi wa mahakama na  lakini wajumbe wa baraza hilo walipuuza na kusisitiza kuwa ni lazima wajitete na walalamikaji waliamua kutoka nje ya mkutano,” alidai Rashid.
Alidai kwamba siku hiyo hiyo kabla ya uamuzi wa kuwafukuza, wakili wake  aliyemtaja kwa jina moja la Panya mnamo saa 9:05 mchana,  aliwasilisha nakala ya uamuzi huo wa mahakama ofisi ya  makao makuu ya chama hicho Zanzibar.

Aliongeza kuwa licha ya kuwasilisha taarifa hizo kwa wakati katika ofisi za chama hicho na kwa Katibu Mkuu na katika mkutano huo wa baraza kuu, baraza hilo liliendelea na azma yake ambayo hatima yake ilikuwa ni kuwafukuza uanachama wa chama hicho.
“Hatua ya  wa walalamikiwa kuendelea na mkakati wao wa kuwafukuza uanachama walalamikaji ulifanyika saa 9:55 jioni, wakati tayari kulikuwa na amri ya mahakama iliyokuwa imeshawasilishwa kwa walalamikiwa,” alizidi kudai.

Katika hati ya dharura iliyoambatanishwa kwenye maombi yao hayo, walalamikaji hao wanadai kuwa kwa kuzingatia uamuzi huo usio halali, walalamikaji wamewasilisha barua kumfukuza uanachama Rashid kwa Spika wa Bunge kwa ajili ya utekelezaji.
Wanadai kuwa ikiwa Bunge litatekeleza jukumu lake wapiga kura wa jimbo la  Wawi, ambao mbunge wao ni mlalamikaji wa kwanza wanaelekea kunyimwa haki yao ya uwakilishi bungeni.

Mbali na Hamad Rashid wengine waliofukuzwa uanachama CUF ni Doyo Hassan Doyo, Shoka Khamis Juma na Juma Saanane, wote wakiwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho.


UTAFITI NA MIWANI BLOG


MIWANI BLOG imefanya utafiti mdogo kwa kutumia picha hii kujua uzima ya macho yako kwa kuiangalia kwa tatika moja na kisha kielezea nini ulichokuwa unahisi wakati ulipokuwa unaitazama picha hiyo. Maji ya kila aliyeona yatafaitiwa na majibu sahii ya utafiti wa picha hii uliyofanya na Mr MIWANI.
Hii ni sehemu ya kuijua afya yako kwa kufanya maaoezi madogo kama hayo na kuweza kupata ushauri kupitia wataalamu wa afya ya binadamu walio na uhusiano wa karibu na miwani blog.


kumbuka kutoa maoni yako juu ya unachokiona hapo ili kuweza kupata majibu sahihi baada ya kutazama picha hiyo


Na Abdulkarimu H. Muro
                                                         New Delh - INDIA 

SAKATA LA UUZAJI UDA VIGOGO WAHOJIWA




SAKATA la uuzaji wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), limezidi kupamba moto baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh, kuwataja vigogo wapya waliohojiwa na shirika lake kutokana na kutajwa kwamba walishiriki katika mchakato wa uuzaji wa hisa za shirika hilo.Akizungumza na Mwananchi jana,  Utouh aliwataja vigogo hao ambao alisema baadhi wameshahojiwa kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba na Mkurugenzi wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena.

KUBENEA AREJEA DAR

Mkurugenzi wa Mwanahali SAED KUBENEA arejea jijini Dar es Salaam kutokea Nchini INDIA alipo kuwa akitiwa. Mmiliki huyo wa gazeti la Mwanahali aliyefanyiwa upasuaji mdogo wa macho siku chache zilizopita katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delh nchini INDIA ambapo alikaa kwa siku siku tano. SAED KUBENEA anatarajiwa kuwasili jijini kesho mchana 11/01/2012 kutekea New Delhi - India. Imeripotiwa kuwa SAED KUBENEA alifanyiwa upasuaji huo ulichukua zaidi ya masaa tatu, huku taarifa za daktari zikielewa kuwa hali yake ni nzuri. akiwa na baadhi ya jamaa na mariki waliomtembea katika hospital hiyo. Picha zifuatazo na matukio

Saed Kubenea akiteta jambo na mmoja wa watanzania Abdulkarim Hussein Muro anaosoma New Delhi nchini India katika uwanya wa ndege wa kitaifa wa New Delhi kabla kuondoka kureja Tanzania 

Picha kulia na kushoto ni Saed Kubena akiwa na marafiki wa karibu wanaoishi nchini India New Delhi ambao walikupata fursa ya kuwa pamoja nae kwa wakato wate aliopo india kwa matibabu yake huku akionekana kuwa na furaha zaidi kurejea nyumbani.

Picha ikumuonyesha Kubenea akiagana na marafiki waliomsindikiza Airport kurejea Tanzania kuoka India              
                                                            kwa mataibabu zaidia


                                                  picha na Abdulkarimu H. Muro
                                                        New Delh INDIA 

KUBENEA AREJEA DAR

Mkurugenzi wa Mwanahali SAED KUBENEA arejea jijini Dar es Salaam kutokea Nchini INDIA alipo kuwa akitiwa. Mmiliki huyo wa gazeti la Mwanahali aliyefanyiwa upasuaji mdogo wa macho siku chache zilizopita katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delh nchini INDIA ambapo alikaa kwa siku siku tano. SAED KUBENEA anatarajiwa kuwasili jijini kesho mchana 11/01/2012 kutekea New Delhi - India. Imeripotiwa kuwa SAED KUBENEA alifanyiwa upasuaji huo ulichukua zaidi ya masaa tatu, huku taarifa za daktari zikielewa kuwa hali yake ni nzuri. akiwa na baadhi ya jamaa na mariki waliomtembea katika hospital hiyo. Picha zifuatazo na matukio

Saed Kubenea akiteta jambo na mmoja wa watanzania Abdulkarim Hussein Muro anaosoma New Delhi nchini India katika uwanya wa ndege wa kitaifa wa New Delhi kabla kuondoka kureja Tanzania 

Picha kulia na kushoto ni Saed Kubena akiwa na marafiki wa karibu wanaoishi nchini India New Delhi ambao walikupata fursa ya kuwa pamoja nae kwa wakato wate aliopo india kwa matibabu yake huku akionekana kuwa na furaha zaidi kurejea nyumbani.

Picha ikumuonyesha Kubenea akiagana na marafiki waliomsindikiza Airport kurejea Tanzania kuoka India                
                                                            kwa mataibabu zaidia


                                                  picha na Abdulkarimu H. Muro
                                                        New Delh INDIA 

Saturday, 7 January 2012

SAID KUBENEA AREJEA INDIA

Mmiliki wa gazeti la Mwanahali amerejeshwa Nchini India kwa kuangalia afya yake, Taarifa zilizotufikia kutoka kwa mwakilishi wetu wa MIWANI BLOG lilifika hospitalin hapo na kuweza kufanya maojiano nae.
Kubenea aliwasilia nchini India tarehe 2/1/2012 majira ya asubuhi na kufikia katika hooteli ya sky Rich iliyo New Delh Karol Baghk.
na kuripoti hospitalini siku iliyofuata.
Baada ya kuripoti hospitali., kubenea alifanyiwa vipimo vidogo ambavyo vilimlazimu kufanyiwa upasuwaji mdogo wa macho uliochukuwa muda wa masaa matano na kuruhusiwa.

Saidi Kubenea akifanyiwa vipimo vidogo  

Picha ni Saidi Kubenea akipelekwa katika chumba cha upasuaji na mmoja wa wauguzi
katika Hospital ya Apolo iliyopo India New Delhi

 Saidi Kubenea akiwa katika kibaskeli cha kubebea wagonjwa
akiwa na mmoja wa wauguzi wa hospital ya Apolo iliyopo nchini India huku akiwa katika usimamizi wa Madaktari bingwa wa macho. Hapa ndipo hospitali alipokuwa akipatiwa huduma hiyo ya macho tangu awali na hali yake kwa sasa ni nzuri na anaendela na dawa. Habari zaidi zinasema hali yake ya mwanzo na sasa ni tofauti kwani Daktari amelieleza MIWAN BLOG kuwa  vipimo vinamridhisha na anamruhusu kurejea nyumbani kwani tayari ameshamfanyia upasuaji mdogo wa macho yake mawili.
 Picha ya kulia inamuonyesha Saidi Kubenea akiwa
katika mapumziko baada ya kufaniwa upasuaji mdogo wa macho yake katika chumba no 204 cha kupumzikia wagonjwa cha Apolo

Saidi Kubenea akifanyiwa vipimo vya mapigo ya moyo baada ya kutoka katika uperesheni 


Tuesday, 3 January 2012

MMM


Tuesday, January 3, 2012

BREAKING NEWS: MADAKTARI WA HOSPITAL YA TAIFA MUHIMBILI WAANZA MGOMO LEO

Dr. Masele Lucas akizungumza leo
Baadhi ya Madaktari na Wafamasia wanaofanya Kazi kwa Mafunzo kwa mkataba wa mwaka mmoja hospitari ya Taifa Muhhimbili wakiwa katika mkutano na viongozi wa Wizara ya Afya na hospitali hiyo Dar es salaam leo baada ya kugoma kwa kutolipwa posho zao kwa mda wa mwezi mmoja
Dr. Flank Kagolo akimwaga cheche zake
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Taifa Muhimbili Dkt. Mariana Njelekelo (kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Madaktari na Wafamasia wanaofanya Kazi kwa Mafunzo kwa mkataba wa mwaka mmoja katika hospitari hiyo ambao waligoma baada ya kukosa mshahara wa mwenzi mmoja Dar es salaam leo
Baadhi ya Madaktari na Wafamasia wanaofanya Kazi kwa Mafunzo kwa mkataba wa mwaka mmoja hospitari ya Taifa Muhhimbili wakiwa katika mkutano na viongozi wa Wizara ya Afya na hospitali hiyo Dar es salaam jana baada ya kugoma kwa kutolipwa posho zao kwa mda wa mwezi mmoja

MWANAMUZIKI WA SENEGAL YOUSSOU NDOUR KUWANIA URAIS

Mwanamuziki mashuhuri nchini Senegal na mwanaharakati wa kisiasa,Youssou N'dour, ametangaza kuwa atawania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi Februari nchini humo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa anaitikia wito wa kumtaka agombee kiti hicho dhidi ya rais wa sasa Abdoulaye Wade, ambaye anapania kuwania kiti hicho kwa muhula wa tatu.
Youssou N'dour amehusika na maswala ya kibinadamu kwa siku nyingi na pia ni balozi wa shirika la umoja wa matataifa kuhusu maswala ya watoto (UNICEF).
Mwandishi wa BBC mjini Dakar, Thomas Fessy, anasema hatua ya bwana Youssou N'dour kutangaza kuwa atawania kiti cha urais, haijawashangaza wengi. Hii ni kufuatia tangazo alilotoa mwisho wa mwaka uliopita kuwa atajitosa katika ulingo wa kisiasa.
Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia kituo chake cha redio na televisheni, mwanamuziki huyo amesema atapunguza matumizi ya serikali na kuahidi kuzalisha chakula na umeme kwa wote iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Senegal.
''kuwa rais ni kazi sio taaluma''
Youssou N'dour anakubali kuwa yeye sio msomi lakini anaelezea wadhifa wa rais kama ''kazi na sio taaluma''.
Youssou N'dour alikuwa rafiki wa karibu wa rais Abdoulaye Wade, lakini baada ya Wade kutangaza nia ya kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu, aligeuka na kuwa mpinzani wake mkuu.
Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Bw. Youssou Ndour kuwabadili maelfu ya wafuasi wake wa muziki kumpigia kura.
Aidha, Youssou N'dour amewahi kuwashutumu viongozi wa nchi za Afrika kuhusu jinsi walivyoshughulikia janga la njaa nchini Somalia.

Miss University Kenya 2012


Tuesday, January 3, 2012

Miss University Kenya 2012

We are happy to introduce Tanzanian beauty, Precious John, the current Miss United States International University (USIU) for 2011. As we speak she is vying for the Miss University Kenya 2012 crown as one of the hottest contenders. OUR appeal to all WADAU u is to promote our very own Sister.
Please vote for Precious as votes will count 60% of total marks. It will be a pride for our Nation if the Crown is won by a Tanzanian abroad. Voters should open www.pambazuka.co.ke.
The big day for the event will be 20th January, 2012 in Nairobi, Kenya, likewise the voting date ends on that day. Voters are allowed to vote every 12 hours.